<big>K</big>ickshaw inakubali vipengele vya XML vifuatavyo na majina ya sifa, thamani za sifa, na yaliyomo yanayohusishwa na vipengee hivi:

<tt><b>Kipengele:</b>			<b>Majina ya sifa:</b>
menu           		id, label, icon, execute
separator      		label
item           		label, icon
↳action        		name
 ↳prompt       		<i>haihusiki</i>
 ↳command      		<i>haihusiki</i>
 ↳startupnotify		<i>haihusiki</i>
  ↳enabled     		<i>haihusiki</i>
  ↳icon        		<i>haihusiki</i>
  ↳name        		<i>haihusiki</i>
  ↳wmclass     		<i>haihusiki</i>

					<b>Thamani za sifa:</b>
action         		Execute, Exit, Reconfigure,
               		Restart, SessionLogout

					<b>Yaliyomo:</b>
enabled        		yes, no</tt>

ID za menyu zinazojumuisha tungo tupu ni halali, lakini kama ID nyingine yoyote ya menyu zinaweza kuonekana mara moja tu kwenye menyu.

— — —

Menyu zifuatazo ni sawa na zote mbili zinakubaliwa na Openbox na Kickshaw.

<tt><b>(1)</b> &lt;openbox_menu&gt;

      &lt;menu id="menu1" label="Menu1"&gt;
        &lt;item label="item"/&gt;
      &lt;/menu&gt;

      &lt;menu id="root-menu"&gt;
        &lt;menu id="menu1"/&gt;
      &lt;/menu&gt;

    &lt;/openbox_menu&gt;</tt>

<tt><b>(2)</b> &lt;openbox_menu&gt;

      &lt;menu id="root-menu"&gt;
        &lt;menu id="menu1" label="Menu1"&gt;
          &lt;item label="item"/&gt;
        &lt;/menu&gt;
      &lt;/menu&gt;

    &lt;/openbox_menu&gt;</tt>

Menyu kila wakati huonyeshwa ndani ya Kickshaw kama itakavyoonekana kwenye Openbox, kwa hivyo mfano wa pili wa mifano miwili upo karibu zaidi na mbinu ya WYSIWYG. Upande mbaya ni kwamba kwa menyu kubwa, hii inaweza kufanya faili ya menyu ionekane inavuruga kiasi. Kwa sababu hiyo, kwa kaida Kickshaw kila wakati huhifadhi menyu katika muundo wa kwanza (hii inaweza kubadilishwa ndani ya michaguo).

Wakati wa kuhifadhi faili, programu hutumia tabu kwa ajili ya majongezo kwa kaida, lakini kwa kusoma faili, ikiwa majongezo kama hayo yalifanywa kwa nafasi au tabu haina umuhimu, vivyo hivyo nafasi nyeupe yoyote.

— — —

Menyu inaweza kuwa na sifa zinazopingana za menyu, kama kwenye mfano ufuatao:

<tt>&lt;openbox_menu&gt;

  &lt;menu id="menu1" label="outside" icon="out.jpg" execute="out" /&gt;

  &lt;menu id="root-menu"&gt;
    &lt;menu id="menu1" label="inside" icon="in.jpg" execute="in" /&gt;
  &lt;/menu&gt;

&lt;/openbox_menu&gt;</tt>

Katika hali hii, Kickshaw hufuata mfano wa Openbox na huonyesha thamani ya sifa ya icon kutoka ndani ya menyu shina, wakati huonyesha thamani za sifa za label na execute kutoka nje ya menyu shina.
